Posts

Showing posts from November, 2025

Kocha matola azungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao dhidi ya JKT Tanzanian

Image
  Kocha Matola kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania.

Zipo timu mbili za Tanzania kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo ni Azam FC pamoja na Singida Black Stars.

Image
  Zipo timu mbili za Tanzania kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo ni Azam FC pamoja na Singida Black Stars. Unamuona Nani Ana Nafasi Kubwa Ya Kuchukua Ubingwa Huu Endapo Akifika Fainali?  1⃣➡️ Singida BS  2⃣➡️ Azam FC

Shirikisho la Mpira wa Miguu la kimataifa (FIFA) limetangaza kuanzisha Tuzo ya Amani ya FIFA (FIFA Peace Prize),

Image
  Shirikisho la Mpira wa Miguu la kimataifa (FIFA) limetangaza kuanzisha Tuzo ya Amani ya FIFA (FIFA Peace Prize), ambayo itatolewa kwa mara ya kwanza wakati wa droo ya Kombe la Dunia Desemba 5, 2025 huko Washington. Kwa mujibu wa FIFA, tuzo hiyo itatambua matendo ya kipekee ya kuleta amani. Hata hivyo, rais wa FIFA Gianni Infantino, ambaye ana uhusiano wa karibu na Rais wa Merekani, Donald Trump, alikataa kufichua kama kiongozi huyo ndiye atakayekuwa mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo. “Desemba 05 mtajua,” amesema Infantino alipokuwa akizungumza kwenye America Business Forum mjini Miami, muda mfupi baada ya Trump kuhutubia mkutano huo huo.

Moussa camara goalkeeper wa simba kuikosa mechi ya kesho dhidi ya JKT .

Image
 “Tutamkosa golikipa Moussa Camara lakini wachezaji wengine wote wapo kambini na wapo tayari kwaajili ya mechi. Hii inatupa jeuri na matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa kesho” 🎙️ Seleman Matola kuelekea kwenye mechi ya kesho dhidi ya JKT Tanzania. kocha huyo ameongea na wanahabari akiwataarifu washabiki na wapenzi wote wa simba kuwa wamejianda vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi hiyo itakayochezwa kesho majira ya saa 1 usiku.

Bryan mbeumo katangazwa mchezaji bora wa mwezi oktoba ligi kuu ya england.

Image
   Baada ya kufunga mabao matatu na pasi moja ya goli, Bryan Mbeumo ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba wa Ligi Kuu England 🏆🇬🇧 Ni mara yake ya kwanza kabisa kushinda tuzo hiyo. Pia mchezaji huyo amesajiliwa kutoka timu ya Brentford alipokuwa akiichezea timu hiyo kwa misimu kadhaa na baada ya man united kuona uwezo wake ikamsajili mshambuliaji huyooo matata kutokea timu ya Brentford.