Shirikisho la Mpira wa Miguu la kimataifa (FIFA) limetangaza kuanzisha Tuzo ya Amani ya FIFA (FIFA Peace Prize),

 





Shirikisho la Mpira wa Miguu la kimataifa (FIFA) limetangaza kuanzisha Tuzo ya Amani ya FIFA (FIFA Peace Prize), ambayo itatolewa kwa mara ya kwanza wakati wa droo ya Kombe la Dunia Desemba 5, 2025 huko Washington.


Kwa mujibu wa FIFA, tuzo hiyo itatambua matendo ya kipekee ya kuleta amani. Hata hivyo, rais wa FIFA Gianni Infantino, ambaye ana uhusiano wa karibu na Rais wa Merekani, Donald Trump, alikataa kufichua kama kiongozi huyo ndiye atakayekuwa mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo.


“Desemba 05 mtajua,” amesema Infantino alipokuwa akizungumza kwenye America Business Forum mjini Miami, muda mfupi baada ya Trump kuhutubia mkutano huo huo.

Comments

Popular posts from this blog