DR Congo imeendelea kuziamini ndoto zake za kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa 4-3 kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Nigeria jana usiku

 



DR  Congo imeendelea kuziamini ndoto zake za kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa 4-3 kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Nigeria usiku wa Jumapili, mchezo uliochezwa mjini Rabat, Morocco, baada ya sare ya 1-1 katika dakika 120 za mchezo wa fainali ya mchujo wa Afrika.


Nigeria ndiyo iliyoanza kupata bao kupitia Frank Onyeka katika dakika ya 3, kabla ya Meschack Elia kuisawazishia DR Congo dakika ya 32. Baada ya mchezo kumalizika bila mshindi hadi dakika 120, nahodha Chancel Mbemba alifunga penalti ya ushindi na kuipeleka “The Leopards” kwenye mchujo wa kimataifa utakaofanyika Machi nchini Mexico.


Comments

Popular posts from this blog