CURAÇAO YAANDIKA HISTORIA: NCHI NDOGO ZAIDI KUFUZU KOMBE LA DUNIA
CURAÇAO YAANDIKA HISTORIA: NCHI NDOGO ZAIDI KUFUZU KOMBE LA DUNIA
Curaçao imeweka rekodi mpya kwa kuwa nchi ndogo zaidi kuwahi kufuzu Fainali za Kombe la Dunia baada ya kulazimisha sare ya 0-0 dhidi ya Jamaica katika siku ya mwisho ya kufuzu kwa ukanda wa CONCACAF. Kisiwa hicho kidogo chenye watu takriban 156,000 pekee kimeibuka kinara wa Kundi B kwa pointi 12 bila kupoteza mchezo wowote, na kuvunja rekodi ya Iceland ya mwaka 2018.
Timu hiyo inayonolewa na Dick Advocaat, kocha mkongwe aliyeongoza Uholanzi na timu kadhaa za kitaifa, ilipata ushindi mkubwa wa 7-0 dhidi ya Bermuda katika safari yao ya kuelekea hatua ya fainali.

Hakikisha unaachia comment hapa chini wadau wa soccer
ReplyDelete